Sunday, February 26, 2012

VIJANA KENYA WAPIKWA KUSAIDIA AL- SHABAAB SOMALIA, WACHINJANA WENYEWE KWA WENYEWE

*Mzazi aeleza jinsi mwanae alivyokuwa na usongo wa kujiunga na Al-Qaeda.
*Mzazi mwingine amshangaa mwanae kudai kwenda vitani Somalia wakati hajui lolote kuhusu vita hivyo.

Bi. Asha Mohamed, mkazi wa Pumwani nchini Kenya, alikuwa amekaa kwenye chumba chake kidogo huku akiiangalia kwa huruma picha ya mwanae, Harun(15) aliyekuwa kwenye vazi la sekondari.

Ilipofika Septemba, Dogo aliyeyuka. Bi. Asha anasema: ‘Siku hiyo Harun aliamka mapema, akamuuliza dada yake, saa ngapi saa hii?’  Aliendela kumuuliza tena na tena na ilipofika saa 10 alfajiri, mtoto wangu akaishia’.

Harun: 'Imetoka hiyoo'
Bi. Asha alijua Harun alipokwenda na kwa kudhibitisha hilo alipokea ujumbe mfupi kupitia simu yake ikithibitisha kuwa, Harun alishavuka mpaka na kujiunga na Al Qaeda ambao ni mabinamu wa Al Shabaab.

‘Alianza kunisumbuasumbua toka akiwa na miaka 14, alikuwa akisema: ‘Mama, mi nakwenda Somalia kupigana vita ya Jihad.’ Nilimpotezea kwa kuwa nilikuwa naona kama anatania vile’ alisema Bi. Asha.

Kwa muda sasa, Al Shabaab wamekuwa wakishawishi Wasomali waishio nje ya nchi yao kuliunga mkono kundi hilo, hali inayoendelea kudhoofisha uwezekano wa kupata serikali ya pamoja. Inadaiwa baadhi ya vijana wa Kikenya, sasa  wanachangamkia ‘ajira’ za kumwaga zinazotolewa na kundi hilo na kuzidi kuchafua hali ya hewa nchi Somalia na mataifa jirani .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni,  inasema: ‘Kuna mtandao wa Wakenya wanaokula meza moja na Al-Shabaab, ambao sio tu kwamba unadoneti mahela ili kusaidia kundi hilo lakini pia unaendesha mafunzo.’

Mafunzo mengi ya ‘wapiganaji’ hawa yanafanyika kwenye makazi yasiyopimwa ya Pumwani, Nairobi.

Al Shabaab kibaruani
Inaelekea vijana wa Kenya bado hajaona kama hili ni tatizo. Inadaiwa marafiki sita wa Harun nao wametokomea Somalia.

Serikali za vitongoji za Pumwani bado hazilizungumzii sakata hili bayana, lakini zinakubali kuwa ‘bwawa limeingiliwa na luba’.

Vijana wa Kikenya walio Somalia, sasa wanachapana na kumwagana damu na kaka zao ‘Jeshi la Kenya’, ambalo kwa miezi kadhaa sasa lipo kwenye ardhi ya Somalia, likijaribu kulifyeka kundi la Al Shabaab linaloundwa na vijana kadhaa toka Kenya. [Chanzo: Mashirika]