Friday, February 24, 2012

TEMEKE QUEENS WALIA NA UKATA, WAOMBA SAPOTI YA WADAU

KIONGOZI mwandamizi wa Timu ya netiboli ya Temeke, Temeke Queens, Amina Mussa, ameomba wakazi wa Temeke na wadau wa michezo kwa ujumla, wajitokeze kuisapoti timu ya netiboli ya Temeke, Temeke Queens, iliyo kambini kujiandaa na kinyang’anyiro cha netiboli ligi daraja la pili kinachotegemea kuanza kuunguruma kuanzia kesho kwenye viwanja nya sigara, Jijini Dar es Salaam.

Amina: 'Wadau mko wapi?'
Akizungumza katika mahojiano maalum na blogu hii, Amina amesema, pamoja na kuwa kambi inaendeshwa kimkandamkanda, lakini bado wachezaji wana hari na wanafanya mazoezi kwa kujituma. ‘Hali si nzuri, tunadaiwa ada sh. 150,000, hela ya vitambulisho sh. 60,000 na posho za wachezaji’, alisema Amina.

Amina ameomba wadhamini kujitokeza kuidhamini timu hiyo ambapo alisema gharama za maandalizi za jumla ni milioni mbili.

Temeke Queens kama wenyeji wa mashindano, wanategewa kushuka dimbani kesho kupambana na wenyeji wenzao timu ya Bandari ambapo Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Bi. Tunu Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.