Friday, February 24, 2012

TANZANIA, CONGO NGUVU SAWA

Ilunga wa Congo(jezi nyeupe) v  Hussein Javu
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imetoka suluhu na Wakata Mayenu, Congo katika mchezo kirafiki unaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii. Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya mapambano ya timu hizo kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika, nchini Afrika Kusini, ambapo Taifa Stars itamenyana na Msumbiji na Congo itakutana na Sychelies. Katika mchezo huo ambao Stars hawakuonesha kiwango cha kuridhisha, uliisha bila nyavu kutingishika. [Picha Full Shangwe]