Wednesday, February 29, 2012

TAIFA STARS OSO KWA USO NA MSUMBIJI TAIFA LEO, NIZAR KHALFAN KUCHANGAMSHA SAFU YA KIUNGO

KIKOSI cha Tanzania, Taifa Stars, leo kinashuka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kuikabili Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2013, nchini Afrika Kusini.

Stars inategemea kungarishwa na kiungo wa kimataifa, Nizar Khalfan na kuhakikisha inawanyima raha Machinga hao wa Msumbiji.
Nizar

Pamoja na kwamba Stars itakuwa ikicheza nyumbani, lakini bado imekuwa ikiteswa na Msumbiji, kwani kumbukumbu zinaonesha kuwa, mwaka 2007 Stars ililala mapema kwa goli la mkongwe, Tico-Tico na safari ya kusonga mbele ikagota hapo. Nyota huyo safari hii hajajumuishwa, amepisha damu changa.

Stars - Tupeni raha
Uwapo wa Nizar utasaidia kuimarisha safu ya kiungo ya Taifa Stars ambayo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Congo iliyochezwa hivi karibuni, ilionekana kuwa nzito hasa inaposhambulia.

Nae Kocha Poulsen ambaye ‘chakula’ chake kitakoma Juni, mwaka huu, amewaomba Watanzania kujitokeza na kushangilia kwa nguvu ili kuwatia morali wapiganaji wa Stars.
Mambaz wanatarajiwa kushusha uwanjani bunduki zao zote ili kutafuta upenyo wa kwenda Afrika Kusini.

Mara ya mwisho Stars kucheza na Machinga hao ilikuwa Aprili 23, mwaka jana kwenye gemu ya ufunguzi wa Uwanja wa taifa wa Zimpeto, Msumbiji. Mshambuliaji Jerry alicheka na nyavu za Stars mara mbili na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Ze Machingaz

Michezo mingine; Ethiopia itaikaribisha Benin, Rwanda itakabiliana na Nigeria nayo Congo itaialika Uganda wakati Burundi itacheza Zimbabwe.
 
Wenyeji Kenya watakutana na akina Adebayor, Togo, wakati Gambia itavaana Algeria, huku Guinea Bissau ikikumbana na wagumu Cameroon, Tchad dhidi ya Wanyasa Malawi nayo Madagascar dhidi Cap Vert wakati Namibia itamalizana na Liberia