Wednesday, February 29, 2012

STARS YAJINYONGA YENYEWE, MCHECHETO WA WASHAMBULIAJI WAKE WAKUTANAPO NA GOLI WAIMALIZA

TIMU za Taifa Stars na Msumbiji zimetoka sare ya mabao 1-1 katika mchezo wa awali wa Fainali za Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam jioni hii. 

Stars ilikuwa na kila sababu ya kuibuka na ushindi mnono, lakini ‘mchecheto’ wa washambuliaji wake waingiapo kwenye boksi ukaiangusha. 

‘Wamakonde’ walikuwa wa kwanza kuandika bao kwenye dakika ya 23 baada ya Clesio Baugue dakika 23 kuiponyoka ngome ya Taifa Stars, akamsogelea Kaseja, akatupia wavuni. Katika dakika ya 42, Mwinyi Kazimoto, aliwainua Watanzania vitini baada ya kufumua shuti kali toka nje ya eneo la hatari lililojaa upange wa kulia wa golikipa Kampangon. 

Matokeo mengine ya michuano hiyo: Madagascar imenyolewa 4-0 na Cape Verde, Rwanda na Nigeria nyavu bado hazijatingishika(mechi bado inaendelea), Ethiopia na Benin 0-0(bado wanakipiga), Burundi na Zimbabwe1-1(bado wanakamuana), Kenya wanaongoza 2-1 dhidi ya Togo(bado wako uwanjani), Chad wameshaikamua Malawi 3-1(Mpira unaendelea), DR Congo wameshacheka na nyavu ya Seychelles mara nne(Bado wako uwanjani) nao Congo Brazzaville na Uganda 1-1(pira unaendelea). Matokea kamili badae kidogo.

Mchezaji Nizar Khalfan wa Taifa Stars(bluu/nyeusi), akichuana na Frasisco Masinga wa Msumbiji ’The Mambas’,  wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika -  Afrika Kusini uliokwisha hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Da es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1. [Picha: FullShangwe].