Thursday, February 23, 2012

NI MPUTU v STARS LEO TAIFA

TIMU ya Taifa (Taifa Stars), yenye wachezaji chipukizi, leo itavaana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars
Wachezaji kadhaa chipukizi wameitwa kuunda kikosi hiko, ambacho pia kitacheza mechi ya kwanza kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (2013) dhidi ya Msumbiji wiki ijayo.

Miongoni mwa sura mpya ni pamoja na Abubakar Salum, Jonas Mkude na Waziri Salum. Kocha Poulsen amesema amewaita kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha kwenye ligi inayoendela.

Nizar Khalfan anayecheza soka la kulipwa na klabu ya Philadephia ya Marekani na Ally Badru wa Canal Suez ya Misri, wao hawatocheza mechi hiyo pamoja na kwamba waliitwa. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwaombea mechi dhidi ya Msumbiji, ambapo wanatarajia kuwasili wakati wowote wiki hii.

Pamoja na chipukizi hao, Stars uzoefu wa nahodha Shedrack Nsajigwa, Nassor Said, Aggrey Moris, Juma Nyoso na Kelvin Yondani.

Wengine ni Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Abdi Kasim 'Babi' Hussein Javu, John Bocco, Mrisho Ngasa, Uhuru Selemani, na magolikipa Shaban Kado, Juma Kaseja na Mwadini Ali.

Tresor Mputu - Kuongoza mashambulizi ya Kongo
 Nae Kocha Msaidizi wa Kongo, Muntubile Santos, alijigamba kuwa wana uhakika wa ushindi.

Pamoja na kukosekana kwa mchekana nyavu hatari, Alain Kaliyutika anayekipiga Qatar, lakini kuwapo kwa nyota wa Tp Mazembe, Tresor Mputu ana hakika mambo yatakuwa safi.

Wakati huo huo, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema, kwa kuwa leo ni siku ya kazi, mchezo huo utachezwa saa 11 jioni. Kiingilio cha chini kitakuwa sh. 2,000 na cha juu sh. 15,000.