Monday, February 27, 2012

MZEE NELSON MANDELA ATOKA HOSPITALINI, NI BAADA YA OPARESHENI

Johannesburg, SOUTH AFRICA

MWANASIASA mkongwe, Veterani, Nelson Mandela(93), ameruhusiwa kutoka hospitalini jana baada ya kufanyiwa operesheni  ya tumbo, kumnusuru na maumivu  yanayomsumbua kwa muda mrefu.

Mzee Madiba
Rasi wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma, amenukuliwa akisema: ‘Madaktari wamemruhusu kurudi nyumbani, kufuatia uchunguzi waliomfanyia na kukugundua kuwa hakuwa na tatizo kubwa linalotishia afya yake’.

Mzee Mandela, kipenzi cha watu, alikuwa kwenye uchunguzi wa kina kufuatia tatizo kiafya la muda mrefu lililodhaniwa kuwa huwenda ni vidonda vya tumbo, magonjwa ya tumbo au henia.

Haikuweza kufahamika mara moja hospitali aliyolazwa, ilifanya hivyo makusudi ili kuepuka umati wa watu ambao ungejitokeza kumjulia hali.

Mzee Mandela, maarufu Madiba, kama anavyoitwa na familia yake, alisota lupango kwa miaka 27 kufuatia kuupinga utawala wa makaburu uliokuwa ukikandamiza ngozi nyeusi  miaka ya nyuma.

Mara ya mwisho, Madiba kuonekana hadharani ilikuwa Julai 2010 wakati wa Fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Habari zinasema, mwaka jana aliwahi kulazwa kwa tatizo la kifua.

 Blogu hii inakutakia Mzee Madiba afya njema. [Chanzo: Mashirika]