Tuesday, February 28, 2012

MIKONO KIUNONI. Mchezaji mkongwe wa Bandari Dar es Salaam, Nuru Fundi ‘Mchina’(WA), akiusubiri mpira kwa hamu huku akilindwa na damu changa za timu ya Tumaini, pia ya Dar es Salaam, Eliza Mbasha(C) na Salome Lazaro, kwenye mchezo mkali wa netiboli Ligi daraja la pili Taifa uliopigwa kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam leo. Bandari ilishinda magoli 36-15. Mechi kadhaa ziliunguruma leo. Temeke Queens imeipeleka mchakamchaka Umoja Queens kwa magoli 36-15, Black Sister ikanyukwa magoli 29-15 na Kurugenzi Tandahimba nao Kambangwa wakapata ushindi kwa taabu wa magoli 23-22 dhidi ya Ras Lindi. Akiongea na blogu hii, Katibu Mkuu CHANETA, Bi. Rose Mkisi, alisema, ligi hiyo inatarajiwa kuendela tena kesho kwa timu kucheza mechi mbili, moja asubuhi na nyingine jioni. Michezo ya asubuhi itazikutanisha Tumaini dhidi ya Kurugenzi, Temeke Queens watacheza na Ras Lindi nao Bandari watavaana na Black Sister. Jioni, Temeke itashuka tena uwanjani kuvaana na Black Sister, Umoja watapepetana na Ras Lindi, Kambangwa na Tumaini watamalizia.

Mmiliki na Mkurugenzi wa Sport FM yenye makao yake makuu Dodoma, Abdallah Majura, akipata mawili matatu toka kwa Katibu wa CHANETA, Bi. Rose Mkisi leo.