Saturday, February 25, 2012

MAMA NURU MIZENGO PINDA KUFUNGUA MASHINDANIO YA NETIBOLI DAR ES SALAAM LEO

MKE wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Nuru Pinda, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano ya netiboli ligi daraja la pili ngazi ya taifa yatakayokuwa yakiunguruma kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam.

Mama Pinda
Akizungumza na blogu hii jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, CHANETA, Bi. Rose Mkisi alisema, jumla timu nane kati ya kumi walizozitemea zimeshawasili Dar es Salaam tayari kwa kindumbwendumbwe hiko kitakachofikia kilele tarehe 3 Machi. 

Alizitaja timu zilizokwisha ripoti kuwa ni; Black Sister (Pwani), Ras Lindi (Lindi), Kurugenzi Tandahimba (Mtwara) na Umoja Queens (Masasi). Kutoka Dar es Saaam ni; Bandari, Temeke Queens, Tumaini na Kambangwa. Timu za Mzinga-Morogoro na moja kutoka Mufindi bado hazijaripoti ila zinatarajiwa kufika wakati wowote.

Bi. Rose alisema timu zinazoshiriki ligi hii zinawakilisha baadhi ya mikoa na kwamba timu itakayoonesha kiwango cha juu na nidhamu itapandisha hadi daraja la kwanza.

‘Ligi hii pia tutaitumia kuchagua wachezaji watakaoongeza nguvu kwenye timu ya taifa ya netiboli iliyoweka kambi Kibaha kujiandaa na mashindano ya netiboli Kombe la Afrika’, alisema Bi. Rose.