Friday, February 24, 2012

MAANDALIZI NETIBOLI LIGI DARAJA LA PILI TAIFA YAPAMBA MOTO

Bi. Rose Mkisi, Katibu wa CHANETA, wa pili kushoto, akifuatilia mazoezi ya timu za Temeke Queens na Umoja Queens za Temeke na Masasi,  hazipo pichani kwenye viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam leo. Wengine toka kulia ni Katibu Muhtasi CHANETA, Bi. Mercy Rehani, Mjumbe Kamati ya Utendaji CHANETA, Bw. Juma Rajab. Kushoto ni kiongozi wa Temeke Queens, Bi. Amina Mussa.
 
MAANDALIZI: Kiongozi wa Temeke Queens ya Dar es Salaam, Bi. Amina Mussa mwenye  filimbi shingoni akifurahia jambo na wapiganaji wa Temeke Queens kwenye mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na michuano ya netibili ligi daraja la pili ngazi ya taifa kwenye viwanja vya Sigara leo.
 
Kocha wa timu ya Masasi Queens mwenye nguo nyeupe katikati, akifuatilia mazoezi ya wachezaji wake.
 
   FULL MAANDALIZI: Wachezaji wa Umoja Queens wakijifua.