Monday, February 27, 2012

LIGI NETIBOLI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA YAPAMBA MOTO DAR ES SALAAM

Katibu wa Michezo Bandari Dar es Saam, Kenny Mwaisabula(kulia), akiteta na Kocha wa timu hiyo, Rose Walele(mwenye kofia), wakati wa mchezo baina yao na timu ya Tandahimba ya Mtwara uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Sigara, Dar es Salaam. Wana-Dar es Salaam walishinda magoli 46-15.

UREFU MALI. Pilly Kassim(GA) wa Kambangwa, akipambana na  Scola Mbuya(GD) wa Temeke Queens, zote za Dar es Salaam kwenye mchezo mkali uliofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu za Kambangwa na Temeke Queens wakichuana. Mechi zingine zilizochezwa leo, Ras Lindi imeshinda magoli 26-13, Tumaini ya Dar es Saalm ikaikandamiza Umoja Queens ya Masasi, magoli 48-14 wakati Bandari Dar es Salaam, ikaidungua bila huruma,Tandahimba magoli 46-15.
AYAAAH!!! Ndivyo anavyoonekana kusema mchezaji wa Temeke Queens, Scola Mbuya(GD), baada ya Pilly Kassim(GA), kurusha mpira(haupo pichani) golini katika mchezo wa Ligi daraja la pili Taifa, uliofanyika kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Grace Tongoli(GS) wa Kambangwa.  Temeke Queens, waliwadungua Kambangwa magoli 24-16.