Saturday, February 25, 2012

LIGI NETIBOLI DARAJA LA PILI TAIFA YAANZA RASMI DAR ES SALAAM LEO, MAMA TUNU PINDA ATAFUNGUA RASMI

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Nuru Mizengo Pinda(kushoto), akifurahia keki maalumu kabla hajaikata kuashiria ufunguzi wa mashindano ya netiboli Ligi daraja la Pili ngazi ya Taifa jijini Dar es Salam leo. Kushoto kwake ni mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais, Mama Zakia Bilal, anayefuatia Mama Lukuvi, Bi. Flora Kasambala(aliyejikinga na kofia)  na kulia ni Mwenyekiti CHANETA, Mama Bayi.

Katibu Mkuu wa CHANETA, Bi. Rose Mkisi, akiongoza shughuli za uzinduzi wa ligi ya netiboli daraja la pili Taifa kwenye viwanja vya Chang’ombe, Jijini Dar es Salaam leo.

Mbunge wa Masasi, Mh. Elizabeth Kasembe(kushoto), akiserebuka na wachezaji wa Kurugenzi Tandahimba ya Mtwara wakati wa gwaride la ufunguzi la ligi ya netiboli daraja la pili taifa iliyoanza Jijini Dar es Salaam leo.

Mchezaji Subira Songwe(GS) wa timu ya Taifa ya netiboli, akijaribu kumuadaa mchezaji wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi katika mchezo wa maonesho uliochezwa kusheherehesha ufunguzi wa Ligi daraja la pili ngazi ya Taifa, Dr es Salaam leo. Wengine katika picha ni; Irene Elias(GA) na Betty Kazinja(C) wa timu ya Taifa, Vero George(GD) na Tulizo Joseph(C) wa Filbert Bayi

Baadhi walezi wa CHANETA, viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, viongozi wa timu shiriki, wageni waalikwa na wadau wa netiboli waliohudhuria ufunguzi huo.