Thursday, February 23, 2012

CHELSEA KUIMALIZA ARSENAL, WAMTOLEA MACHO WINGA WALCOTT

KLABU ya Arsenal, huwenda wakajikuta kwenye wakati mgumu zaidi kwenye Ligi kuu ya Uingereza msimu huu, baada ya jana kuchomoza taarifa kuwa, Chelsea inamfukuzia kwa udi na uvumba wingi mwenye kasi wa Washika Bunduki hao, Theo Walcott.
Walcott - Njoo Chelsea


Walcott mwenye thamani ya paundi milioni 10, amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake, Sturridge yeye ni mpaka 2014.

Babu wa Asenal, Arsene Wenger, kwa siku za karibuni ameonekana akihaha kutafuta mshambuliaji na hivi karibuni alionekana kumzungumzia Sturridge. 

Walcott, 22, ameonekana kutaabika msimu huu, hata hivyo Wenger amepanga kumwongezea mkataba.

Wenger amekuwa akilalamikiwa na kutakiwa kuongeza ‘mavumba’ kwa wachezaji angalau paundi 100,000 kwa wiki — kiwango ambacho Chelsea imekuwa ikilipa ‘wanajeshi’ wake kitambo. [Chanzo: Mashirika]