Wednesday, February 15, 2012

CELINE DION: UNGA, KUJIRUSHA NA WAPAMBE NUKSI VIMEMMALIZA


Kujirusha? Aku! - Celine
MWANAMUZIKI nyota wa Kimarekani, Celine Dion (43), anaamini, dawa za kulevya, makundi mabaya na ubendera fuata upepo ndivyo vilivyofupisha maisha ya Whitney Houston.

Nyota huyo ameyanyooshea kidole  maisha ya  ‘kujirusha’ na athari zake na kudai anayaogopa na hataki kuyasikia.

Celine aliyetamba na kibao, ‘My Heart Will Go On’, amesema: ‘Maisha ya kujirusha yananiogopesha. Naogopa ‘unga’. Naogopa kujiachia usiku. Ma-pati simaindi, sijirushi. Na ndio maana mimi si sehemu ya ‘wauza sura’, inatubidi tuogope staili hiyo ya maisha’.

Celine ameongeza kusema: ‘Inasikitisha kuona unga, aaah sijui…wapambe au vishawishi vimechukua maisha ya Whitney. Vimezima ndoto yake, vimechukua upendo na maisha yake kama mama’.

Nae Mwimbaji, Annie Lennox, 57, amekifananisha kifo cha Whitney na janga au zahma. ‘Alijaliwa kila kitu – mrembo, kipaji cha pekee, maarufu na tajiri. Lakini unaposhindwa kubalansi maisha/kazi/umaarufu na mbaya zaidi ukamiksi na unga, ni sawa na kubwiasumu kali. Wanamuziki wengi maarufu wameuvaa huo mkenge’, amedai Annie.