Saturday, February 25, 2012

BINTI MIAKA TISA AFA BAADA YA KUHENYESHWA MCHAKAMCHA KWA SAA TATU MFULULIZO


Savanna
WAKATI jitihada mbalimbaili zimekuwa zikichukuliwa duniani kuwalinda watoto na ukatili, Mtoto Savannah Hardin, miaka 9, mkazi wa Alabama, amepoteza maisha baada ya kupewa adhabu ya kukimbia kwa saa tatu bila kupumzika. Bibi na mama wa kambo wa marehemu ndio vinara wa unyama huo na sasa wanakabiliwa na kesi ya mauaji.

Shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Roger Simpson alisema: ‘Nilimwona binti mdoogo akikimbia nje ya nyumba anayoishi, nikaendelea na hamsini zangu’.

Mamlaka zinasema, Mtoto Savannah Hardin alipoteza maisha baada ya kupewa adhabu ya kukimbia kwa saa tatu bila ‘kuomba maji’ baada ya bibi yake kufura kufuatia na mjukuu wake huyo kumpiga fiksi kwamba hakula ‘pipi’.

Savannah alipungukiwa maji kwa kiasi cha kutisha na alifariki siku chache baadae. Jumatano iliyopita, polisi iliwatia mkononi bibi na mama wa kambo wa marehemu kwa kosa la mauaji.

Bibi(kushoto), Maza(kulia)
Mashuhuda waliviambia vyombo vya dola kuwa, siku ya Ijumaa, Savannah alipigishwa mchakamchaka kwa saa tatu mfululizo na hakuruhusiwa kusimama. Polisi wanasema ilipofika saa12:45 jioni, mama wa kambo wa Savannah, Jessica Mae Hardin(27), alipiga simu polisi akiwataarifu kuwa, ‘mwanae’ alikuwa hajitambui. 

Polisi ikawakuwanya wote wawili. [Chanzo: Mashirika]