Tuesday, February 28, 2012

BANDARI DAR YAENDELEA KUTESA LIGI YA NETIBOLI DARAJA LA PILI TAIFA

Katibu wa Michezo Bandari Dar es Salaam, Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’, akifurahia kiwango kilichokuwa kikioneshwa na ‘wapiganaji’ wake wa timu yake wakati ilipokuwa ikiumana na Tumaini pia ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Sigara Jijini Dar es Salaam, jioni hii. Kushoto kwake ni Mhariri wa gazeti la Spoti, Masoud Sanani.
AMKA TWENDE MAMA: Kocha wa Timu ya Tumaini, Ubwa,  akimpa sapoti mchezaji wake, Anna Msulwa, baada ya kupata maumivu. Hata hivyo mchezaji huyo alishindwa kuendelea na mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Bandari na Tumaini zote za Dr es Salaam, wakichuana katika mchezo wa kusisimua uliopigwa jioni hii kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa ligi netiboli daraja la pili Taifa. Bandari imeendeleza ushindi kwa ushinda magoli 36-15. Picha na matokeo zaidi ya ligi hiyo baadae kidoooogo.