Thursday, February 23, 2012

ASHLEY COLE AMKOSOA KOCHA, KIBARUA CHAKE KUOTA NYASI CHELSEA

BILIONEA na mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, amechukizwa na kitendo cha beki wa timu hiyo, Ashley Cole kukosoa laivu mbinu za ufundishaji za kocha wake, Andre Villas-Boas. 
Abramovich: 'Cole chezea mimi ee?'

Mtu wa ndani wa klabu hiyo amesema: ‘Mchezaji akimkosoa kocha ni sawa na kukosoa maamuzi ya mmiliki’.

‘Kocha Andre Villas-Boas ni chagua binafsi la Abramovich. Mara nyingi wachezaji maarufu huwatunishia misuli makocha wasio na majina’. Safari hii Bosi kachoshwa na sokomoko zao’, amesema.

Gazeti la SunSport, Jumatano iliyopita, liliandikwa kuwa, nyota Cole, Frank Lampard na Michael Essien walitupwa benchi kwenye mechi na  Napoli kutokana na kumkosoa AVB.
Cole alimpasha laivu kocha wake kuwa, kwa staili yake ya ufundishaji, kamwe wasitegemee kikombe chochote.

Cole: 'Villas-Boas anatuyeyusha'Pamoja na upepo kuwaendea vibaya Cole na wenzake hata hivyo kocha wao naye amekalia kuti kavu, uwezo wake wa kufundisha unatiliwa shaka.

Cole, 31, na Lampard, 33, mikataba yao itakwisha mwaka 2013 lakini ikifika usajiri wa majira ya joto, watawaweka sokoni.