Wednesday, February 29, 2012

ANYONGA MKE KISA KAZAA ‘BEBI GELO’, MAMA AMPIGA TAFU MWANAE KUUWA

Kunduz, Afghanistan.
Waliosema tembea uone, hawakukosea! Polisi kaskazini ya Afghanistan jimbo la Kunduz, wanamsaka kwa udi na uvumba mume anayesemekana kuuwa mkwe wake baada ya kumzaa mtoto wa kike kwa mara ya tatu na sio wa kiume.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi nchini humo ilisema, Bw. Sher Mohammed, 29, alimwoa Storay(22) miaka minne iliyopita

Wanandoa hao walibahatika kupata watoto wa k ike watatu ambapo wa mwisho aliyeleta sokomoko ana miezi mitatu toka azaliwe, alisema Mkuu wa Polisi Wilaya ya Khanabad, Chifu, Sufi Habib.

Baada ya kujifungua mtoto wa kike, Bw. Mohammed alimkoromea mkewe kwa kushindwa kuleta ‘dume’. ‘Hatimae Jumamosi iliyopita, mume akisaaidiwa na mama yake mzazi akamtwanga mkewe vya kutosha kasha akamkaba mpaka mama wa watu akapoteza uhai,’ alisema Chifu huyo.

Polisi wanamshikilia mama mzazi wa mtuhumiwa, Bi. Wali Hazrata, aliyesweka kwenye jela ya mji wa Kunduz city jail. Mume kala kona na hajulikani aliko. Akihojiwa na polisi, Bi. Hazrata alijijitetea na kusema kwamba, mkwewe alijiua bila sababu.

Bi. Wali Hazrata
‘Aaah, mnituwe, mwanangu hajauwa…! Baada ya kujifungua watoto wa kike mara tatu mfululizo, Storay alijisikia mkosaji na akaamua kujimaliza,’ alidai Bibi huyo.
Taafifa hii imekuja baada juzi baada ya polisi wa Afghan, kumwokoa binti wa miaka 15, aliyekuwa amefungiwa ndani bila ya chakula kwa anti yake huku kucha zake zikiwa zimenyofolewa.

Msichana, Sahar Gul, aliolewa na njemba moja la miaka 30 mwaka jana, mamlaka ya Kaskazini mwa Baghlan, inasema binti huyo alifanyiwa ukatili huo baada ya kukataakata kata  kujihusisha na biashara ya kuuza mwili.

Pamoja na utawala wa Taliban kupigwa chini, wanaharakati nchini humo wanasema bado kuna maeneo wanawake wanaendelea kukiona cha mtema kuni kila kukicha.

Kwenye robo ya pili, mwaka jana, Afghan Independent Human Rights Commission (AIHRC) inadai kurekodi matukio 1,026 ya vichapo kwa wanawake. 2010, vipigo vilipaa kufikia 2,700.
Disemba mwaka jana, ‘mwehu’ mmoja akiwa na silaha, aliimwagia familia moja tindikali baada ya familia hiyo kumnyima binti mdogo.

Katika tukio lingine la mwaka, Bi.Gulnaz(21), amehukumia miaka 12 jela baada ya kuripoti polisi kuwa binamu wa mumewe alimbaka.

Hata hivyo dada huyo aliachiwa baada ya wanaharaka kuingilia. Ili kuepukwa kusimangwa zaidi na jamii yake, masikini amekubali achukuliwe jumla na ‘mbakaji’ kwani tayari ana kiumbe chake tumboni. Kuachiwa kwake pia kulichangiwa na Rais wa Afghanistan, Bw. Hamid Karzai 
kuingilia kati.

Bi. Horia Mosadiq, mtafiti mwenye asili ya Afghanistan anayeishi Uingereza na kufanya kazi na Amnesty International,amesema kitendo alichofanyiwa Storay Mohammed vinawakuta wanawake wengi.

‘Kwa ujumla haki za binadamu na hasa za wanawake hazizingatiwi. Nimekuwa nikifanya kazi na vikundi vya kutetea haki za wanawake karibu nchi nzima, wanasema ukatili umekuwa ukiongezeka kila kukicha,’ alisema mtafiti huyo.

Ameongeza kusema matukio yanaongezeka kufuatia wanawake kupata elimu kuhusu haki zao na wanapokwenda kuzidai kwenye familia zao hapo ndipo ‘moto’ unapowaka.

Mila inathamini sana mtoto wa kiume. Mtoto wa kiume anachukuliwa kama ‘kitu cha thamani’, amasema, ukizaa mtoto wa kike ni kama umezaa ‘msiba’, hakuna sherehe.

‘Ili hali ya wanawake wa Afghan ziweze kulindwa kunahitajika nguvu za kisiasa na msaada toka jamii ya kimataifa.women is to improve,’ amesema Mosadiq.

‘Wakati mabapo jamii ya kimataifa imejikita kwenye masuala ya migogoro ya kivita imefika wakati sasa pia iweze kutupia macho watu wa Afghan na hasa wanawake. [Chazo: Mashirika]