Thursday, February 23, 2012

AMA KWELI, MAJI HUFUATA MKONDO. MTOTO WA WHITNEY HOUSTON AFUMWA ‘AKIJIDUNGA’

BOBBI KRISTINA HOUSTON, 18, binti wa Mwanamuziki Whitney Houston, amefumwa akijidunga baada ya mazishi ya mama yake, imeelezwa. 

Bobbi Kristina - Mwanampotevu
Bobbi, alikutwa hotelini tayari akiwa ‘anabembea’ baada ya kutoweka. Ndugu akiwemo Bibi yake, Cissy(Mama wa Whitney), walihaha huku na kule walijaribu kumpigia lakini hawakumpata.

Lakini baada ya kupatikana na ikionekana anaficha tatizo, Bibi Cissy alisema kuwa, mjukuu wake hana tatizo, yuko kamili gado.

Nae msemaji wa familia alisema: ‘Bobbi anahitaji mapumziko, yu bukheri wa afya’.

Whitney, 48, alifariki huko Los Angeles hivi karibuni.